Tuamke katika masuala ya Fedha za kidigitali

in #tuamke8 years ago

Mimi ni mtanzania ninayependa mageuzi haya makubwa ya fedha za kidigitali. Tokea mwaka jana nilipoanza kujifunza habari za bitcoin hakika nimepata uelewa wa kutosha kuwasaidia wengine kujua jinsi mapadiliko haya yanavyoweza kutuletea manufaa makubwa ya kiuchumi. Hivyo wito wangu ni kuwa japo wengi hawajui kiingereza, basi sisi tunaojua tuwasaidie. Naamini hili jukwaa la Steemit litatufaa sana hata sisi tunaotumia kiswahili kama lugha yetu kuu.
Wanaofahamu kiswahili tutumie lugha hii kama inakubalika, kuwakilisha ujumbe kwa wote wanatumia kiswahili

Ninafurahi sana kuwakaribisha waswahili wenzangu popote walipo duniani tudumishe lugha yetu na pia tutoe makala mbalimbali katika Steemit ili kukuza uchumi wetu

Kwa maoni zaidi nawakaribisha kuyatoa.

Wenu Geofrey

Sort:  

mimi si mswahili lakini najua kiswahili kidogo kuomba maji tu. tujifunze na tukazane pamoja